Home SPORTS YANGA OUT, UHAI CUP

YANGA OUT, UHAI CUP

Kikosi cha Yanga B kimeondolewa kwenye mashindano ya Uhai Cup chini ya miaka 20 baada ya kwenda sare na Mbeya City ya 1-1 kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Chuo Kikuu mjini Dodoma (UDOM).

Yanga imeondoshwa kwa sare hiyo ambapo katika jumla ya mechi zake zote ilizocheza imeshindwa kupata ushindi na ikiondoka bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Katika kundi A, Yanga imemaliza ikiwa nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya Mbao na Ruvu Shooting ambazo zimetinga hatua kucheza robo fainali.

Kwa matokeo ya sare hiyo, Yanga imeungana pamoja na Mbeya City kuyaaga mashindano hayo kwa kuwa na alama moja pekee kwenye kundi A.

Aidha, katika kundi C, klabu ya Azam imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa kuilaza Mwadui FC kwa mabao 2-1.

Mechi za kundi B zinakamilishwa kesho ambapo Singida United na Njombe Mji, wakati Simba SC watakuwa wanacheza na Stand United.

Kundi D litawakutanisha Kagera Sugar na Tanzania Prisons huku Ndanda akicheza na Lipuli.